Shirika la PACT Tanzania linalotekeleza mkakati wa USAID na ACHIVE leo 20/05/2022 limeikabidhi Manispaa ya Ubungo pikipiki moja yenye no ya usahili DFPA 9047 kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa Ustawi katika kutekeleza shughuli za Ustawi wa Jamii.
Akiongea katika tukio hilo Ndugu Bariki Amani Mbwambo Afisa Tathmini na ufuatiliaji wa shirika la PACT- ACHIEVE amesema shirika hilo linaisadia jamii kujenga uwezo wakuzalisha kipato, kupata huduma bora za afya na kutumia rasilimali zilizopo ili kujipatia kipato.
Aidha Mbwambo ameeleza sambamba na mengi wanayoyafanya katika kuisaidia jamii hivyo wameamua kugawa pikipiki hiyo kwa ajili ya kutekeleza shughuli za Ustawi wa jamii hususani kwa watoto na hivyo kuwarahisishia Maafisa Ustawi kuweza kufuatilia kwa ukaribu maslahi ya watoto kwa Jamii.
Akiongea Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt. Peter Nsanya ametoa shukrani kwa shirika hilo kwa kuamua kuisaidia Jamii kwa namna hiyo na kusema kuwa pikipiki hiyo itaenda kurahisha sana utendaji kazi kwa Maafisa Ustawi katika kuhakikisha ustawi wa watoto unaimarika.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa