Naibu Waziri Ofisi ya Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) David Silinde, ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kutekeleza kwa haraka agizo la Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli la kuitaka Manispaa hiyo kuhakikisha wanafunzi wa shule ya King'ongo wahakai chini wala kusomea nje baada ya taarifa za upungufu wa miundombinu katika shule hiyo hiyo kurushwa kwenye mitandao ya kijamii.
Silinde ametoa pongezi hizo leo januari 23 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa madarasa 9 na choo chenye mafundi 12 katika shule hiyo na kueleza kuwa ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa maradi huo ambapo kwa muda wa Siku tano madarasa hayo yamefikia hatua ya linta, hongereni kwa kutii agizo la Mhe. Rais kwa haraka.
Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi king'ongo Manispaa ya Ubungo ukiwa hatua ya linta
"Kufanikiwa kufikia hatua ya linta ndani ya Siku tano kwa madarasa tisa yanayojengwa hapa shule ya msingi King'ongo, inatoa tafsiri tosha kuwa viongozi tunauwezo wa kutekeleza miradi ya serikali kwa wakati tukiamua na tukidhamilia" amesema lusinde.
Amesisitiza kuwa, Kwa kasi hii kumbe darasa linaweza kukamika ndani ya mwezi mmoja lysine amesema hakuna sababu ya kuchelewesha miradi kwani inawezekana kukamilisha kwa wakati kama walivyofanya Manispaa ya Ubungo.
Kufuatia agizo la mheshimiwa Rais kwa manispaa ya ubungo, Silinde ameziagiza halmashauri zote nchini zenye wanafunzi wanakaa chini au kusomea nje kuhakikisha wanaanza ujenzi wa madarasa pamoja na utengenezaji wa madawati ili kuhakikisha changamoto hiyo inamalizika kabisa kwa wanafunzi wa sasa na kuwa na mipango kwa ajili ya mwaka ujao kwani idadi ya wanafunzi itaongezeka kutokana na fursa ya elimu bila malipo.
Akitoa taarifa mbele ya Naibu waziri OR-TAMISEMI Mhe David Silinde, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amesema, Manispaa inaendelea kutekeleza agizo la mhe Rais ambapo ujenzi wa madarasa 9 unaendelea na kufikia januari 31, 2021 madarasa yatakuwa umekamilika pamoja na madawati na wanafunzi wataanza kuyatumia rasmi tarehe 5 februari, 2021.
Amesema kujenga madarasa pamoja na madawati haitoshi, hivyo Manispaa ya nimeamua kujenga choo chenye matundu 12, mradi huu hadi kukamika kwake utagharimu jumla ha shilingi milioni 205 zote kutoka mapato ya ndani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic (wa pili kulia) akitoa maelezo ya utekkelezaji wa agizo la mhe Rais la kujenga madarasa kwa haraka katika shule ya msingi King'ongo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa