Taasisi za serikali zatakiwa kwenda na wakati kwa kutumia mifumo ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Hayo yamesemwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius John Ndejembi kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha 3 cha Serikali Mtandao.
kikao kazi hicho kinachofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha - AICC, kimejumuisha wadau mbalimbali kutoka Serikali kuu, Serikali za mitaa, Mashirika ya Umma na sekta binafsi.
Hayo pia yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro katika kusisitiza kwa kuzitaka taasisi za serikali kwenda na wakati kwa kupunguza matumizi ya karatasi kwa kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA iliyopo katika shughuli mbalimbali za kila siku.
Pia Dkt. Ndumbaro alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha washiriki wa kikao kazi hicho kuhuisha taarifa zao zilizopo kwenye Tovuti ziendane na wakati na kuboresha Mitandao ya kijamii.
Katika kikao kazi hicho cha 3, wataalamu kutoka Manispaa ya Ubungo wanashiriki.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa