Maafisa kilimo Manispaa ya Ubungo leo tarehe 29/3/2021 wapigwa msasa kuhusu elimu ya kilimo rejea cha Viazi na Mihogo na Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania - TARI ( Tanzania Agriculture Reserch Institute) kilichopo Kibaha
Lengo la mafunzo rejea hayo ni kuwajengea uwezo maafisa ili kutoa huduma ya ugani stahiki kwa wakulima katika uzalishaji inayopelekea kuongeza tija katika kilimo biashara na ukuaji wa uchumi na viwanda
Aidha mwezesha wa mafunzo hayo Dk Ester Masumba alisema kuwa ni vyema kufata kanuni na sheria zinazohusiana na kilimo iliuzalishaji uwe wa kiwango cha juu
Esther aliendelea kwa kuwaasa wataalam kuhakikisha wanazingatia matumizi ya mbegu sahihi na zenye ubora mashambani na kufuata hatua za kilimo bora ili kupata mazao kwa wingi
Aidha Bi.Hildelitha Msita Meneja wa TARI aliwasisitiza wataalam kuhakikisha wanazingatia mafunzo hayo ilikuimalika zaidi katika kilimo
Sambamba na hayo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Manispaa ya Ubungo Happness Mbelle aliushukuru uongozi wa TARI na kuomba kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya watafiti na wagani kwa maendeleo zaidi katika maswala ya Kilimo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa