Mwanamitindo na mjasiliamali wa kike Falaviana Matata leo katika ukumbi wa Serena hotel jijini Dar es salaam amezindua ufadhili wa taulo za kike 1000 kwa wasichana wanaoishi katika mazingira magumu katika shule za sekondari na msingi kwa nchi nzima kupitia taasisi yake inayojulikana kwa jina la Flaviana Matata Foundation.
Aidha Matata alisema kuwa Kwa nchi nzima taasisi hiyo imetoa taulo za kike za LAVY 1000 ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam zimetolewa taulo 250 ambazo zitatolewa bure kwa kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kuanzia ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Pia alisema kuwa taasisi hiyo ilianzishwa ikiwa na lengo la kumsomesha mtoto wa kike wanaotoka katika mazingira magumu pamoja na kuhamasisha upatikanaji wa elimu bora katika mazingira rafiki na salama kupitia utoaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, ujenzi na ukarabati wa vyoo,madarasa ,ofisi za nyumba za walimu
Sambamba na hayo alitoa maelezo mafupi kutokana na jitihada za taasisi hiyo zikiwa zinalenga kutatua na kuwapa moyo na kuwajengea ujasiri watoto wa kike na kujiamini wanapokuwa katika masomo yao hata kipindi wanapokuwa katika siku zao.
Aliendelea kwa kuwaomba taasisi,makampuni na mashirika binafsi kuungana na taasisi ya Flaviana matata Foundation kuweza kusaidia kufikia wanafunzi wengi zaidi wanaoishi katika mazingira magumu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa