Tarehe 8/9/2020 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo *Beatrice Domic* amepokea ugeni wa Timu ya tathimini na ufuatiliaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kwaajili ya kutembelea ujenzi wa jengo la Utawala la Ofisi za Manispaa ya Ubungo lililopo Luguruni.
Aidha Mkurugenzi alitoa ufafanuzi wa mradi ulipofikia na alisema kuwa kasi ya ujenzi wa mradi ni ndogo na kupelekea kuchelewa kukamilika kulingana na muda uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe.Aboubakar Kunenge* alipotembelea mradi huo na kutoa wiki sita kwa Mkandarasi wa TBA kuhakikisha mradi umekamilika.
"Mpaka sasa imebaki wiki moja na mradi bado haujakamilika na wafanyakazi hawapo site" Aliongeza Mkurugenzi
Pia Mkurugenzi alisema kuwa tumekazana baadhi ya vitu vimalizike kwa kutumia force account ili sehemu ya chini ya jengo hili iweze kukamilika kwa haraka kwaajili ya shughuli za uchaguzi mkuu ziweze kufanyika.
Sambamba na hayo Wakaguzi walimshauri mwanasheria wa manispaa kumwandikia barua ya onyo wakala wa majengo (TBA) ili aweze kuongeza kasi ya kuendeleza mradi huo"
Wakati wakiendelea na ukaguzi katika sehemu mbalimbali za jengo hilo Wakaguzi walishangazwa na idadi ndogo ya vibarua ambao wapo kwenye mradi.
NB.Timu ya Ufuatiliaji na tathimini inatembelea Miradi ya Kimkakati iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam na kwa Manispaa ya Ubungo imeanza na ujenzi wa jengo la Utawala na kumalizia na ujenzi wa Soko la Mburahati kesho kutwa tarehe 10/9/2020
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa