Timu ya Wataalamu ya Manispaa ya Ubungo (CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo imetembelea na kuona utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Dar es salaam inayojengwa Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo ambapo kwa sasa mradi upo hatua ya boma.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya uboreshaji elimu ya sekondari (SEQUIP) ambapo kwa awamu ya kwanza Manispaa hiyo imepokea Bilioni 3 Kati ya Bilioni 4 kutoka Serikali kuu, ambazo zimepangwa kutumika kwa ajili ya kutekeleza Mradi huo ambao unatekelezwa na wakandarasi wawili ambao ni Bandiko Construction Limited na Valosu Construction Limited.
Mradi huo kwa awamu ya kwanza unajumuisha ujenzi wa vyumba vya Madarasa 12 pamoja na Vyoo vitatu, Ofisi 3, Maabara 4, Bwalo, Mabweni matano, Jengo la Utawala, Nyumba tatu za walimu, Matanki ya maji, kichomeo taka, mitaro ya maji, Uzio, Barabara za watembea kwa miguu na vyoo matundu 16.
Akiongea baada ya ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Beatrice Dominic amemtaka Kaimu Mhandisi wa Manispaa hiyo kutoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ikihusisha changamoto na ongezeko la gharama kwenye Mradi (valuetion) na namna ya kutatua changamoto hizo ili mradi ukamilike kwa wakati
Sambamba na hayo Beatrice ameitaka Idara ya manunuzi na Kitengo cha Mhandisi kuhakikisha kuwa wanawajibika ipaswavyo katika kutekeleza majukum yao ili kuepukana na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Mmoja wa Wakandarasi wanaojenga mradi huo kutoka Kampuni ya Bandiko Construction Limited amesema wao kama wakandarasi wa Mradi huo wapo tayari kushirikiana na Manispaa katika kuhakikisha Mradi huo unakamilika kwa viwango na muda uliokusudiwa.
@ortamisemi
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa