- Mapema leo Novemba 16, 2022 timu ya wataalamu wa Manispaa ya Ubungo ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Dkt. Peter Nsanya imetembelea miradi miwili ya ujenzi wa Madarasa
- Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa vyumba 11 vya madarasa katika shule ya sekondari Urafiki pamoja na ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa katika shule ya Sekondari Makoka
- Timu hiyo imetoa maelekezo kwa mafundi pamoja na kamati za ujenzi za shule hizo kuongeza kasi ya ujenzi ili kufikia lengo la kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ifikapo Disemba 15
- Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na mapokezi ya jumla ya fedha shilingi Bilioni 1.62 kutoka kwa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kujenga vyumba 81 vya Madarasa kwa wilaya ya Ubungo kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kuanza masomo yao mwezi Januari 2023
@tamisemi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa