Hayo yalikuwa maneno ya Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ubungo Ezra Guya wakati wa kikao na Shirika la Centre For Science and Environment kutoka India.
Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Luguruni na kuhudhuriwa na *Naibu Meneja wa mradi Dr. Sonia D. Henam na wataalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Akizungumza Afisa Mazingira alisema Manispaa ya Ubungo hutumia asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwenye suala zima la usafi lakini kama tukiweza kuzitunza vizuri na kuzitumia taka ngumu zinazooza basi tunaweza kupata mapato kwa kuziuza kwenye masoko yanayozihitaji na hatimae kuongeza mapato.
Aliongeza kuwa taka ngumu zipo kwani hata Manispaa ya Ubungo inazalisha wastani wa tani 880 kwa siku. Hivyo kwa kushirikiana na Shirika la CSE baada ya kikao cha pili utekelezaji utaanza wa kuzihifadhi na kuzitumia taka hizo kwa matumizi mengine yatakayofaa.
Nae Naibu Meneja wa Shirika la CSE alisema kuwa kuna ongezeko la wananchi kutoka vijijini kuja mjini la asilimia 0.6 kila mwaka jambo ambalo pia linasababisha taka kuongezeka. Hivyo aliishauri Manispaa ya Ubungo kuliangalia hili kwa jicho la pili ili lisipate madhara yoyote yale na kutumia njia za kisasa kuhifadhi na kutumia upya taka ngumu.
*”Tayari CSE tumeshafanya kazi na NEMC na Zanzibar jambo ambalo limeleta matokeo chanya na tumeona kuna umuhimu wa kufanya kazi na Ubungo ndio maana tupo hapa’’* Aliongeza kaimu Meneja.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa