Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg. James Mkumbo amefungua semina ya wajasiriamali wa Wilaya ya Ubungo iliyofanyika ukumbi wa Mbezi Luxury uliopo Mbezi. Katibu Tawala alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano imetoa maelekezo kwa Wilaya zote kutoa mkopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na Wilaya ya Ubungo inatekeleza hilo. Alisema lengo la mafunzo haya ni kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha hizi ambazo zinaenda kutolewa, tuzitumike kwa ajili ya kupata maendeleo kwa ufasaha kwani nia ni kila linaloenda kufanyika liwe na faida kwetu. Pia semina hii itawawezesha wajasiriamali kufanya matumizi sahihi ya fedha hizi zinazotoka Halmashauri ili waweze kuzirejesha na vikundi vingine viweze kufaidika nazo. Wajasiriamali wengi wataweza kujua namna nzuri ya kuweka kumbukumbu zao maana mali bila daftari hupotea bila habari. Kwa robo ya kwanza mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri imetoa kiasi cha Tshs. Milioni 693,950,000 kwa vikundi 150 kutoka Kata zote 14 zinazopatikana Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo"* alisema Katibu Tawala. Pamoja na hayo aliwakumbusha kwamba unaporejesha vizuri mkopo ndio unavyojiongezea mwanya wa kupata zaidi wakati mwingine na dhumuni kubwa la serikali yetu ni kutoa mkopo usio na riba na hii yote ni kuwawezesha watu wote wapate kwa urahisi na muweze kurejesha, "Tufanye haya kwa kuzingatia marejesho ya mikopo hii kwani itasaidia hata kwa wengine kuweza kupata mikopo hii , turejeshe ili na wengine wanufaike pia na fedha hizi"*. Alisema Katibu Tawala.
Katibu Tawala aliiagiza Manispaa kuhakikisha inatoa fedha hizo za uwezeshaji kila robo kama sheria na taratibu zinavyotaka na aliwaasa vijana wajitokeze kwa wingi zaidi kwani inaonekana vikundi vya wanawake ndio vina uelewa mkubwa na vinafaidika zaidi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa