Hayo yalikuwa maneno ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori wakati akipokea madawati kutoka kwa wahisani wa NMB katika Shule ya Sekondari Kibamba.
Benki ya NMB imetoa jumla ya madawati 150. 50 kwa Shule ya Sekondari Kibamba, 50 kwa Shule ya Sekondari Kinzudi na 50 kwa Shule ya Msingi Kibamba. Katika shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inafanya makusudi kuinua sekta ya Elimu chini ya Rais wa awamu ya tano Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutoa elimu bure. Mkuu wa Wilaya pia alimsifu Mhe. Rais kwa mamlaka aliyo nayo kwa kusimamisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa sababu ya ugonjwa unaosambaa wa Corona.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ambaye pia ndio Mganga Mkuu wa Manispaa alitoa uelewa juu ya kirusi cha Korona. Aliwaomba wanafunzi, walimu, wazazi na wajumbe kutokushikana mikono lakini pia kufuata masharti ambayo yeye kama Mganga Mkuu ameyatoa. "Niombe kila sehemu kuweka maji ya kutiririka maeneo ya kuingia na kutoka ili tuisaidie serikali kuepukana na janga hili" alisema Mganga Mkuu.
Wakati akifunga Meneja wa NMB kanda ya Pwani Ndg. Badru Iddy alisema wao kama NMB wako bega kwa bega na Mhe. Rais ili kufikia Uchumi wa Kati. Vile vile kwa kuwa serikali na wananchi ni wanahisa wa benki hiyo hawana budi kurudisha sehemu ya Faisal wanayoipata kwa wananchi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa