Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mheshimiwa Jaffary Juma Nyaigesha amewapongeza Wakuu wa shule 21 na wasimamizi wote wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 151 kwa usimamizi mzuri wa Miradi hiyo ambapo mpaka sasa ujenzi upo hatua ya kuezeka na umaliziaji na kueleza kuwa kwa kasi hiyo miradi hiyo itakamilika kwa wakati.
Mstahiki Meya ameyasema hayo kwenye kikao cha Tathimini ya ujenzi wa madarasa hayo kilichofanyika leo desemba 03, 2021 kikilenga kufanya tathimini ya ujenzi wa madarasa hayo na kueleza kuwa kazi ina kwenda vizuri, na kuwasisitiza kuzingatia taratibu na mwongozo wa force Account katika utekelezaji wa miradi hiyo.
“Tupo vizuri , tuongeze kasi, tutamaliza kwa wakati nawasisitiza kutumia fedha za miradi hii vizuri sambamba na kutunza vifaa vitakavyobaki” alisisitiza Nyaigesha
Aidha, kipekee, Mstahiki Meya amewapongeza Wakuu wa shule na walezi wa kata wanaojenga Madarasa katika shule za Sekondari za Kimara, Ukombozi, Makabe na Malambamawili kwa kufanikiwa kujenga madarasa pamoja na changamoto ya kijiographia kuwa ngumu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Beatrice Dominic amewasisitiza Wakuu wa shule na walezi wao kuzingatia utunzaji mzuri wa taarifa za mradi kama sheria taratibu na mwongozo ya Force Akounti unavyoelekeza ikiwemo mihutasri ya vikao vya matumizi yote.
Wakitoa taarifa za utekelezaji wa ujenzi wa madarasa hayo Wakuu wa shule na walezi wa kata wamesema wataendelea kusimamia miradi kwa nguvu zote kwa kuzingatia miongozo na sharia na kukabidhi madarasa hayo kati ya tarehe 7 Hadi 10 ya mwezi desemba.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa