Kamati ya Fedha Manispaa ya Ubungo imefanya ziara ya kutembelea Hoteli ya Ubungo Executive Lodge iliyopo kituo cha mabasi cha Magufuli Bus Terminal lengo ikiwa ni kukagua Hoteli hiyo.
Ziara hiyo imefanyika Leo tarehe 27 Oktoba, 2022 ambapo wajumbe wa Kamati hiyo wamefanikiwa kuona vyumba na mgahawa wa Hoteli hiyo.
Akiongea ndugu Emmanuel Saulo Mapolu Meneja wa Hoteli hiyo wakati akielezea gharama za vyumba vya Hoteli hiyo amesema kwa sasa kuna vyumba vya shilingi elfu 30, elfu 40 na vyumba vyenye vitanda viwili ambavyo vina gharama ya shilingi elfu 50.
Mapolu ameendelea kueleza hoteli hiyo ina mgahawa “restaurant”yenye mazingira rafiki kwa wateja na ina jumla ya vyumba vya kulala 39. Na kwa sasa Hoteli itakuwa tayari kuanza kutoa huduma mara tu itakapo zinduliwa.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha amewapongeza wasimamizi wa Hoteli hiyo kwa usimamizi mzuri akiwemo Ndugu Benjamin Fredy Mwandete Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli hiyo pamoja na Meneja wa hoteli hiyo na kutoa wito kwa wananchi kujionea fahari ya kuwa na Hoteli hiyo ambayo itaenda kuchochea maendeleo kwa wana Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa