- Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliotokea katika nchi ya Uganda, Tanzania kupitia Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalim amezitaka taasisi mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo
- Leo Oktoba 5, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amefika katika kituo cha Mabasi cha Magufuli kukagua kituo maalumu kilichowekwa kwaajili ya kufanya uchunguzi kwa wasafiri mbalimbali dhidi ya ugonjwa huo
- Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dokta Peter Nsanya akitoa maelezo ya hatua ambazo tayati wamezichukua amesema kuwa mpaka kufika leo tayari wasafiri 615 wameshachunguzwa afya zao na wote wako salama. Kuna mabasi 14 yanayofanyiwa uchunguzi kila siku ambapo mabasi hayo yanafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoa wa Kagera na Nchi ya Uganda
- DC Kheri ameridhishwa na hatua ambazo zimechukuliwa na idara ya afya ili kudhibiti ugonjwa huo kuingia jijini hapa kupitia Wilaya ya Ubungo
- Aidha DC Kheri ameutaka uongozi wa kituo cha Mabasi cha Magufuli kuwa, asitokee mmiliki yoyote wa Mabasi au mfanyakazi wa basi lolote akakaidi maelekezo hayo yaliyotolewa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa