Manispaa ya Ubungo kwa kishirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ubungo wamefanya kikao kazi kilicholenga kufanya tathimini ya uchambuzi wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato hususani ushuru wa huduma (service levy) kwa Wilaya ya Ubungo kwa kutazama utendaji kazi wake wa mifumo hiyo na kushauri namna bora ya kuongeza ufanisi wa mifumo hiyo na kuzuia mianya ya rushwa.
Hayo yameelezwa Leo Desemba 22, 2022 na Afisa Uchunguzi wa Takukuru Ndg. Mboto David wakati akifungua warsha iliyolenga kuongeza mapato kwa Manispaa ya Ubungo.
Aidha, Bi. Sheira Mleba amesoma taarifa ya uchambuzi wa mfumo wa ushuru wa huduma kwa wafanyabiashara Wilaya ya Ubungo na kubaini changamoto za ukusanyaji wa ushuru na kutafuta suluhu, wajumbe waliweza kupendekeza maoni mbalimbali.
Wajumbe walipendekeza wafanyabishara wapewe elimu kuhusiana na ulipaji wa ushuru wa huduma yaani (Sevirce levy) na uboreshaji wa sheria ndogondogo za Manispaa ambazo zitalenga kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Aidha, wajumbe walipendekeza kufanyike maboresho ya sheria ndogo ambazo zitasaidia kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, sheria hizo ni pamoja na itakayo wabana wafanyabishara wanahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuhakikisha wanahamisha taarifa za biashara zao kwenda kwenye Halmashauri husika ambapo biashara inafanyika kwa sasa
Nae Fredrick Mbigili Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo amewashukuru wajumbe na ugeni kutoka TAKUKURU kwa kutoa ushirikiano mzuri ambao unalenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa mapato wilayani humo.
Halikadhalika, Ndugu Mboto David kutoka Takukuru ameshukuru wajumbe wa kikao hicho na kuagiza utekelezaji wa maazimio na mapendekezo ya kikao yafanyiwe kazi kwa wakati.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa