Kuelekea kilele cha siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16.6.2022, Manispaa ya Ubungo Leo tarehe 15.6.2022 imeadhimisha siku hiyo katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Young Counseling Organization ( YOCO) kilochopo Malamba Mawili kwa kutoa Elimu kwa wanafunzi 120 kutoka katika shule za sekondari na msingi zilizopo katika Wilaya hiyo.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Tuimarishe ulinzi wa mtoto; tokomeza ukatili dhidi yake” tujiandae kuhesabiwa.
Akiongea Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Hanan Mohammed Bafagil amewaasa wanafunzi kuhakikisha wanapopata changamoto za ukatili wa kijinsia, manyanyaso katika familia na hata mashuleni kuwasilisha kwa wazazi au walimu wao na kuwataka Kufika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ili waweze kupatiwa ufumbuzi.
“ Serikali yetu ni sikivu na viongozi wako makini , tunaahidi kutoa ushirikiano bega kwa bega kila mwenye jambo linalomtatiza alifikishe mahali panapostahili ni lazima litafanyiwa kazi” Hanan aliendelea kusisitiza.
Halikadhalika amewashukuru wadau wa Asasi mbalimbali walioshiriki katika baraza la watoto wakiwemo child intimacy,right sight organization, jamii safi salama, the chosen generation na crisis revolving center
Nae mratibu wa baraza la mtoto Manispaa ya Ubungo Bupe Mwansasu ameendelea kuzitaka Asas zilizoshiriki kuendelea kujitoa na kumshukuru Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha YOCO kwa kujitolea kutoa eneo lake kuanzia mwanzo hadi mwisho wa tukio.
Sambamba na hayo zoezi hilo limefanyika kwa kuwapa Elimu yakupambana na matukio ambayo yanawanyima haki zao za msingi, umuhimu wa kupata haki za watoto katika jamii, uongozi na uwajibikaji.
Aidha watoto wameelezea mahitaji yao ikiwemo kupata fursa yakusikilizwa, haki yakuendelezwa, haki yakuishi, haki kwa watoto wakike kupata nafasi yakushiriki michezo kama ilivyo kwa watoto wakiume na haki yakulindwa.
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa