Kuelekea kilele Cha Maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 1, desemba kila mwaka, Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na Asasi zisizo za Kiserikali ikiwemo Konga ya Manispaa ya Ubungo imeadhimisha siku ya ukimwi Kiwilaya katika ukumbi wa mikutano wa TGNP uliopo Mabibo na kutoa misaada kwaajili ya malezi ya watoto ikiwemo Taulo za kike 1224, lishe kwaajili ya watoto na malighafi ambazo vyote kwa pamoja vimegharimu jumla ya shilingi 3,036,000
Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 27.11.2021 yamekwenda Sambamba na Kauli mbiu ya Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI,Tokomeza magonjwa ya Mlipuko
Akifungua Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amezishukuru Asasi zilizo mstari wa mbele na mapambano dhidi ya UKIMWI na kuwataka kueendelea na moyo huo huo
Aliendelea kwa kusema kuwa maambukizi ya UKIMWI hayawezi kumzuia mtu kutofanya shughuli zake za maendeleo na pia nipendelee kuwaasa na watu wengine inapaswa kuwa na utamaduni wa kupima Afya ilikuweza kujua Kama umepata maambuki na kwa wale ambao tayari wanamaambukizi waendelee kuchukua tahadhari
"Tuishi nao kwa upendo watu waliopo kwenye Jamii zetu wenye maambukizi ya UKIMWI, tuwajali na tusiwa nyanyapae" alisisitiza hayo Kheri
Nae Mercy Ndekeno Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Manispaa ya Ubungo ametoa taarifa hali ya kuenea kwa VVU na UKIMWI kwa Wilaya ya Ubungo ni asilimia 2.3 ambalo kiwango kipo chini ya kiwango Cha kitaifa cha asilimia 4.7
Aliendelea kueleza huduma zinazotolewa na Halmashauri katika kusaidia kupunguza maambukizi kwa Wilaya ya Ubungo ambapo kumekuwa na huduma zinazotolewa za upimaji wa VVU kwa hiari na ushauri nasaha katika vituo vya Afya 42 vilivyopo katika Manispaa ya Ubungo
Na pia utoaji wa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) katika vituo 42 ambavyo vinaendelea kutoa huduma hii
Kuratibu kamati za kudhibiti Ukimwi za Halmashauri katika ngazi ya Halmashauri ,kata,mitaa ili ziweze kutekelezwa majukumu yake, Kutoa elimu na huduma ya matunzo kwa watumishi wanaoishi na Vvu , Kutoa elimu ya kudhibiti Ukimwi kwa Vijana walioko mashuleni sekondari na shule za msingi
Alikadhalika kuratibu mashirika na Asasi zisizokuwa za Serikali zinazopambana na kudhibiti maambukizi mapya VVU kwa makundi yaliyokatika Hatari kubwa ya maambukizi
Mwisho, Ndekeno ameendelea kuwashukuru Asasi 20 zinazoshirikiana na Manispaa ya Ubungo kutoka katika Kata 14 wanazoshiriki ipasavyo katika mapambano dhidi ya UKIMWI na Asasi izo ni KONGA,TGNP,STEPS TZ,YOCO,ZITAE,Care for AIDS ,RLST,Center Against GBV n.k
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa