Kuelekea maazimisho ya siku ya wanawake Duniani tarehe 8 Machi 2022, Manispaa a ya Ubungo leo tarehe 4 Machi 2022 wameadhimisha siku ya wanawake duniani kiwilaya katika eneo la Manispaa lililopo Luguruni.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kauli mbiu ya Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, tujitokeze kuhesabiwa sambamba na maazimisho hayo wanawake wa Manispaa hiyo walipata nafasi yakupata elimu mbalimbali ikiwemo elimu ya afya na uzazi, elimu ya kutunza akiba, elimu ya bima ya CHIF n.k.
Akifungua maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amesisitiza wanawake kuendeleza uzalendo wa kuendelea kuwalinda na kuwaongoza vijana na watoto ambao wapo katika jamii zetu kwa kuhakikisha wanapewa misingi bora ya malezi.
“Mtoto wa mwenzio ni wako, kila mmoja anajukumu la kuwafundisha na kuwaongoza” alisema James .
James amesema Falsafa ya kumjali mwanamke ianzie chini kwa kuwajali vijana ambao wanachipukia kwa kuhakikisha wanapewa malezi bora ili waje kuwa kizazi chenye maadili.
Aidha James amesema Msingi wa maendeleo kwa Wilaya ya Ubungo unaletwa na wanawake, Mkurugenzi wetu ni mfano tosha, tujivunie maendeleo yetu yanayosimamiwa vyema na wanawake.
Nafasi ya mwanamke kiuchumi imeendelea kusimamiwa vyema na serikali yetu kwa kumjali Mwanamke katika nafasi mbalimbali ikiwemo uongozi, uchumi n.k
James aliendelea kusisitiza kila mmoja kuwa Wakili wa haki na Usawa katika kupinga unyanyasaji wa kijinsia katika jamii, ofisini na hata shuleni.
Viongozi tengenezeni fursa kwa wengine ambao wangepata nafasi mbalimbali kwa kutumia vyeo vyenu ambao mpo madarakani na wanawake wengine watieni moyo viongozi wenu kwa kuwapa ushirikiano katika kuleta maendeleo.
Halikadhalika, amewashukuru wadau mbalimbali ambao wameshiriki katika kuhakikisha maadhimisho hayo Yanafana wakiwemo TALGWU, CRDB,NMB, DSWU,WYI,HUDEF,RLST n.k
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa