Manispaa ya Ubungo yaadhimisha wiki ya magonjwa yasiyoambukiza tarehe 12, novemba, 2021 kwa kufanya mazoezi ya kutembea na kutoa huduma ya kupima bure kwa wananchi magonjwa yasiyoambukiza ambayo ni presha, moyo, saratani, macho n.k pamoja na kutoa ushauri juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora, na kutoa huduma ya chanjo ya UVIKO 19
Maadhimisho hayo yamekwenda Sambamba na kauli mbiu ya BADILI MTINDO WA MAISHA, BORESHA AFYA yaliyoanzia kwa kutembea kutoka Kituo Cha Afya Cha Kimara Hadi Hospitali ya Wilaya iliyopo Kimara Baruti
Akifungua hafla hiyo Katibu tawala Wilaya ya Ubungo James Mkumbo amewasihi wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kwa kufanya mazoezi kwaajili ya kuimarisha Afya na kuunga mkono jitihada za serikali kwa kupima magonjwa yasiyo ambukiza bure
"Mzingatie ulaji wa vyakula vyenye Lishe bora ili kuimarisha Afya zetu "
Aidha Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic aliwaamasisha wananchi kufanya mazoezi ikiwa ni njia moja wapo ya kuboresha afya na pia kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ambavyo vipimo vinatolewa bure katika eneo hilo
Utoaji wa huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyo ambukiza litahitimishwa kesho tarehe 13.11.2021,wananchi wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa