Ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji dunia kwa muda wa siku saba kuanzia Jana august 1 mpaka agust 7 yakiongozwa na kauli mbiu ya "JUKUMU LETU SOTE" Manispaa ya Ubungo imeadhimisha kwa kupitia kituo Chake Cha afya Cha Mbezi kwa kuongea na wakina mama wanaonyonyesha juu ya kuzingatia lishe Bora kwa afya ya mtoto
Akiongea wakati wa maadhimisho hayo Afisa lishe Manispaa ya Ubungo Beatrice Mosile amewasisitiza wakina mama kuzingatia lishe Bora ya vyakula na kuzingatia masharti yanayotolewa na wataalam wa afya juu ya utunzaji wa afya ya mtoto na pia mama anayenyonyesha
Aidha alitoa elimu ya lishe anayotakiwa mtoto kuipata ikiwemo kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa kipindi Cha miezi sita bila ya kupewa chakula chochote na atakapofikisha zaidi ya miezi sita na kuendelea mtoto anaweza kupatiwa mchanganyiko wa vyakula
" Hakikisha mwanao ananyonya mpaka miaka miwili ili awe na afya bora" alisema Mosile
Kwa mama aliyeathirika na mtoto aliyezaliwa ajapata maambukizwi anashauri kunyonyesha mtoto kwa kipindi Cha mwaka mmoja na kwa aliyepata maambuzi na mtoto akaathirika atanyonyesha kwa muda wa miaka miwili. Aliongeza Mosile
Nae mratibu wa afya jamii Bi.Shubila Bachuba aliwasisitiza kuzingatia maagizo yanayotolewa n idara ya afya kwa Sasa juu ya ugonjwa wa korona kwa kuhakikisha wanafata miongozo ya kujikinga kwa kunawa mikono kwa maji titirika na kuoga wanapokuwa katika mikusanyiko kabla ya kumshika mtoto warudipo majumbani kwa kumlinda mtoto
Sambamba na hayo bi.magret mbena mmoja wa wamama walioshiriki katika uzinduzi wa maadhimisho hayo ameshukuru kwa elimu waliyopata na kuahidi kuzingatia lishe Bora kwa afya ya mtoto wake
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa