Kuelekea kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani tarehe 8 machi, 2023 Wilaya ya Ubungo imeadhimisha siku hiyo leo tarehe 3 machi, 2023 katika viwanja vya Manispaa ya Ubungo vilivyopo Luguruni Kibamba, maadhimisho yaliyoenda sambamba na kauli mbiu ya UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA, CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA
Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashimu Komba akiambatana na viongozi wa Manispaa hiyo wametembelea mabanda mbalimbali ya vikundi vya wakina mama vinavyofanya uzalishaji wa bidhaa
Akiongea katika maadhimisho hayo Komba amesema kuwa Natambua na kuthamini nafasi ya mwanamke katika jamii
Aidha Komba aliendelea kwa kusema kuwa leo tarehe 3 ni siku ya maadhimisho ya Siku ya wanawake Kiwilaya na kazi kubwa katika siku hii ni kutambua mchango wa mwanamke katika jamii hasa katika ulezi wa familia
"Mwanamke ni mama na ni mlezi katika familia" alisema hayo Komba
"Wanawake ni viongozi na niwachapakazi" alipongeza Komba
Mwanamke ni shupavu anayeweza kukusanya mapato vizuri na mwaka huu billion 32 zinakusanywa na mama Shupavu Beatrice Dominic Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
Rais wetu wa awamu ya Sita ni mwanamke hii inaonyesha ni jinsi gani wanawake ni jeshi kubwa na wanaweza, nchi yetu sasa ina kiongozi mwanamama na anaiongoza nchi vyema
"Wanawake pendaneni" hii ni rai yangu kwenu wanawake wote, ubunifu wenu wanamama ni jambo muhimu
Wakina mama mkatoe elimu kwa watoto wetu majumbani kwa kuwaelimisha kuhusina na mambo machafu ambayo sasa yanapamba moto tutoe mwanga kwa watoto wetu wajue mambo haya ni mabaya
Aidha Komba ameipongeza idara ya maendeleo ya jamii ambayo ndo imeendaa maadhimisho hayo kwa kuendelea kusimamia utoaji wa mikopo ambayo haina riba ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Juni 2021/2022 vikundi 747 vya wanawake vimeshapewa mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni 3.8 kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali za uchumi ikiwemo ufugaji, Kilimo, viwanda vidogovidogo, Mama lishe na biashara ndogondogo
Das Ubungo akiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake
Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa