Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewapongeza wafanyabiashara wa Wilaya ya Ubungo kwa kuwa chanzo cha kuboresha huduma kwa wananchi na kukuza uchumi wao kupitia kodi na tozo wanazolipa kwa Halmashauri.
Pongezi hizo amezitoa kwenye kikao kilichofamyika Julai 31, 2022 kati ya wafanyabiashara na Serikali kilicholenga kujadili na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara pamoja na kutoa elimu ya kukuza biashara zao.
Kikao hicho ambacho kinalenga pia kuboresha mahusiano kati ya Serikali na wafanyabiashara ni matokeo ya Mbunge wa jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo baada ya kupokea kero kutoka kwa wafanyabiashara hao na kuahidi kujibu hoja zao kupitia kikao cha pamoja.
Prof. Kitila amesema kuwa wafanyabiashara ndio walipa kodi wakubwa kwa Manispaa ya Ubungo na Serikali hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha wafanyabiashara wanakuwa na mazingira mazuri ya kufanya biashara ikiwemo kuwapa elimu ya ushuru, tozo ada na kodi mbalimbali za manispaa na faida zake kwa jamii.
"Kazi yangu ni kuwa kiungo kati ya Serikali na wananchi na hili nimelitekeleza kwa kuhakikisha kikao hiki kinafanyika ili kufahamu changamoto na kukubaliana namna bora ya kufanya biashara ikiwemo uwepo wa uwazi wa sheria zinazozimamia biashara amefafanua prof. Mkumbo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara Wilaya ya Ubungo ndg. Kelvin Pascali amemshukuru mbunge kwa kutimiza ahati yake lakini pia serikali kufanikisha kikao hiki mhiumu kinachotupa fursa ya kujadili changamoto, fursa na kupata elimu ya kodi hasa zile zinazotutatiza
Kelvin amesema utaratibu huu wa kukutana uwe endelevu ili wafanyabiashara waone fahari kufanyabiashara katika Wilaya hii na hivyo kulipa kodi kwa hiari kama serikali inavyoelekeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amewashukuru wafanyabiashara kwa kushiriki kikao hicho mhimu na kuahidi utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kufanyika kila kata ili kuondoa changamoto ya ufinyu wa elimu kwa mlipa kodi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa