Kamati ya Afya Msingi Ngazi ya Wilaya imekutana kujadili namna itakavyowezesha zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio kwa watoto walio chini ya miaka mitano awamu ya tatu litakalo fanyika kuanzia tarehe 1 - 4 septemba, 2022 ambapo watoto 174,588 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo
Akiwasilisha Taarifa ya zoezi la utoaji wa chanjo kwa awamu ya pili na ya kwanza Mganga Mkuu Manispaa ya Ubungo Dkt. Peter Nsanya amesema kuwa kwa awamu zote mbili zoezi lilifanikiwa na kuvuka lengo ambapo kwa awamu ya pili ilidhamiriwa kuwafikia watoto 168,010 na kufanikiwa kuvuka lengo mpaka kufikia asilimia 113%
Dr Nsanya amesema kuwa katika zoezi la utoaji wa chanjo awamu ya tatu Wilaya ya ubungo ina jumla ya timu 271 zitakazotoa huduma ya chanjo hiyo katika Vituo na nyumba kwa nyumba
Nsanya, aliendelea kwa kusema kuwa chanjo ipo tayari katika Vituo vyote vya Afya na watoa huduma wapo na watapita nyumba kwa nyumba na watakaoenda kwenye Vituo vya kutolea huduma watapata chanjo hiyo.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye ndie Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Kheri James amesisitiza wazazi wenye watoto wanao stahili kupata hiyo chanjo kuhakikisha wanawapeleka kupata chanjo katika Vituo vilivyo Karibu yao
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewasitiza viongozi wa dini na Serikali kuendelea kutoa hamasa Makanisani, Misikitini, masokoni na sehemu zingine ili zoezi liweze kufanikiwa na kufikia malengo.
Sambamba na hayo, Mjumbe wa kamati hiyo Ndg. Feruzi ameipongeza kamati kwa hatua iliyofikiwa na kuhaidi kamati kuendelea kufanya hamasa zaidi ili kufanikisha zoezi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa