Afisa biashara Manispaa ya Ubungo Prisca Mjema amewasihi wananchi wa Manispaa hiyo kujitokeza kwa wingi katika kituo cha mawasiliano Sim2000 kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu ya mlipa kodi na huduma za afya ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya huduma kwa mwananchi .
Prisca ameeleza kuwa, Manispaa ya Ubungo imeamua kumfikia wananchi alipo kwa kusogeza huduma karibu na yake ikiwa mkakati wa kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wake.
"Hili zoezi ni endelevu tulianza kituo cha mbezi na sasa tupo hapa kwenye kituo cha daladala cha sim2000 kwa lengo moja tu la kuhakikisha wananchi anapata huduma kwa urahisi kupitia kaulimbiu yetu ya Ubungo yako inakufikia ulipo, nawakaribisha wote tuwahudumie" anaeleza Mjema.
Mjema alisema kuwa huduma zinazotolewa ni pamoja na ulipiaji wa leseni za Biashara, leseni za vileo, vibali vya ujenzi, vibali vya burudani, ushuru wa huduma , uchangiaji wa damu na ulipiaji wa tozo mbalimbali za Halmashauri. Mjema anasema kuwa 'Wananchi anayefika hapa mfano kukata leseni anapata ndani ya muda mfupi bila kuzunguka kwani huduma zote zinapatikana hapahapa"
Pia katika kituo hiki wananchi wanapata fursa ya kuchangia damu ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhakikisha vituo vyetu vinakuwa na damu ya kutosha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya kutolea huduma huduma za afya
Aisha Mwamfupe ni mmoja wa wananchi walifika kupata huduma katika kituo cha sim2000, ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa ubunifu huo wa kuamua kuwafikia wananchi waliopo Kwa lengo la kuboresha utoaji huduma Kwa haraka zaidi.
" Kupata leseni Kwa Kwa dakika kadhaa sio jambo dogo , naipongeza Sana Manispaa ya Ubungo kwa mkakati wao huu inatija Sana kwa Sisi wananchi hakika Ubungo yangu huduma karibu yangu' anaeleza Aisha mkazi wa kata ya sinza
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa