.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kupata HATI SAFI kwenye ukaguzi wa fedha mwaka 2020/2021 na kuielekeza kufanyia kazi maoni na mapendekezo yaliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG ili kuendelea kupata hati safi.
Mhe. Makalla ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo uliofanyika leo Juni 24,2022 kwa ajili ya kupitia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG na kuwataka Wataalamu na Madiwani kufanyia kazi maoni ya Mkaguzi ili hoja hizo zifungwe.
Aidha, Mhe. Makalla ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kutumia vishikwambi katika kuendesha vikao na mikutano ya Halmashauri.
Pia amesema kuwa "Pamoja na Manispaa hii kuwa changa lakini imekuwa Halmashauri ya kwanza kutumia vishikwambi kama kifaa cha kuendeshea vikao badala ya makabrasha ya makaratasi, nawapongeza sana" alisema
Akisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Mweka Hazina wa Manispaa hiyo Ndugu George Mzeru amesema Manispaa ya Ubungo ilikuwa na hoja 38 ambapo kati hizo hoja 15 zimefungwa huku 23 zikisubiri uhakiki wa mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.
#UbungoYetuFahariYetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa