Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yapokea Mgawanyo wa watumishi ,Madeni na Mali kutoka katika lililokuwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam liliovunjwa na aliyekuwa Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli tarehe 24 Feb,2021
Akiwasilisha taarifa hiyo katika baraza maalum leo tarehe 30 juni, 2021 Mchumi wa Manispaa ya Ubungo Salvius Nkwera aliainisha Mali ambazo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ime pata kuwa ni watumishi 43 , magari 4, pikipiki 1, mitambo 3 na vingine vingi.
Aidha, Manispaa ya Ubungo katika mgao wa ardhi, majengo na viwanja imepata maeneo matatu ya uwekezaji ambayo ni Asphalt plant and fenced Yard, stendi ya mabasi Magufuli (Mbezi Luis) na stendi ya zamani ya Ubungo
Pia Manispaa ya Ubungo imepewa Mashauri 3 Kati ya 21 kutoka Lililokuwa jiji la Dar Es salaam
Katika mgawanyo huo pia Manispaa ya Ubungo imerithi mikataba ya ujenzi na huduma na kurithi Madeni yenye thamani ya shilingi Bil.9.030
Nae Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Jaffari Nyaigesha aliwataka watalaam kuendeleza juhudi hasa katika usimamizi wa miradi na uendeshaji mzuri ili mapato yaweze kuongezeka na kufikia lengo
Pia Mwenyekiti wa chama Wilaya ya Ubungo Ndg.Mgonja aliwaomba watalaam kupitia miradi mikubwa ambayo Ubungo imerithi ikasimamiwe ipasavyo ili mapato yaongezeke
"Niwapongeze kwa kupata Hati Safi kwa miaka Mitatu Mfululizo" alisema Mgonja
Ikumbukwe kuwa baada ya kuvunjwa kwa lililo kuwa jijIa la Dar es Salaam na aliyekuwa Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli aliipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya ilala na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tarehe 24 Feb 2021
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa