Manispaa ya Ubungo, tarehe 25.10.2021 imepokea Vifaa tiba ( mashuka 100,sanitizer 60 pamoja na wheelchair 4 (viti maguru ) kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 toka kuanzishwa kwa chuo hiko
Akipokea Vifaa hivyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ameushukuru Uongozi wa chuo kikuu Cha Dar es salaam kwa jitihada walizoonyesha kwa mchango mkubwa wa vifaa hivyo ambao utawanufaisha wananchi wa Wilaya ya Ubungo
Beatrice, amekipongeza chuo kwa kufikisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa kwake na kwa mchango mkubwa ambao Kituo Cha Afya Cha Kimara kimeupata.
"Vifaa hivi tuna ahidi kuvitunza na kuhakikisha vina dumu" aliongeza Beatrice
Aidha Prof.William Anagise Makamu Mkuu wa chuo Cha Dar es salaam akisoma taarifa fupi ya tangukuanzishwa kwa chuo hicho amesema kuwa chuo kitaendelea kushirikiana na Manispaa ya Ubungo katika kuwaletea manufaa wananchi wa Ubungo na Taifa kwa ujumla.
Aliendelea kwa kusema kuwa katika siku hii ya Maadhimisho ya miaka 60 tangu chuo Kikuu Cha Dar es salaam kuanzishwa itaadhimishwa kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kuendelea kutoa huduma kwa jamii na kutoa ushirikiano kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo
Kwa upande wake Mganga Mkuu Manispaa ya Ubungo Dkt.Peter Nsanya amepongeza jitihada za chuo kikuu cha Dar Es Salaam kwa ushirikiano walio utoa ikiwa ni njia moja wapo ya kuboresha mahusiano mazuri na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Mfawidhi wa Kituo Cha Kimara Dickson Masale ameushukuru Uongozi wa chuo hicho kwa kukichagua kituo hicho kutoa vifaa hivyo kati ya vituo 22 vya serikali vinavyotoa huduma Manispaa ya Ubungo.
Shukrani zingine amezitoa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwa kuendelea kukilea vyema Kituo hicho na kuendelea kuleta matunda zaidi
ReplyForward |
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa