Leo Oktoba 26, 2022 idara ya afya Manispaa ya Ubungo imefanya kikao kazi na baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kinachohusu mambo mbalimbali yanayotekelezwa na idara hiyo ikiwemo mpango wa Afua za Lishe, utayari na namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola pamoja na mpango wa chanjo ya polio.
Akizungumza katika kikao hicho Afisa Lishe wa Manispaa ya Ubungo ndugu Beatrice Mossile amesema kuwa idara ya afya, Ustawi wa jamii na lishe imeendelea kutekeleza afua zake mbalimbali kila siku na kuweza kuleta ufanisi wa kutosheleza pamoja na kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa vituo vya kutolea huduma ya afya.
Kwa sasa idara ya afya inajipanga kutekeleza mkataba wa lishe kwa awamu ya pili uliosainiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan mwezi Oktoba, 2022
Aidha kwa upande wa mpango wa chanjo ya Polio Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inajipanga kufanya awamu ya nne ya kampeni ya Polio ambayo imepangwa kufanyika kuanzia tarehe 3 hadi 6 Novemba, 2022 ambapo walengwa ni watoto 174, 588 chini ya miaka mitano. Akizungumza kuhusu kampeni hiyo Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dokta Peter Nsanya ametoa wito kwa wananchi wa manispaa hiyo kutoa ushirkiano kwa watoa huduma pindi zoezi hilo litakapoanza rasmi kama ambavyo walitoa ushirikiano katika kampeni tatu za awamu zilizopita
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Jaffary Nyaigesha ameipongeza idara ya Afya kwa mipango kazi yote wanayoitekeleza na pia ametoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Ubungo kutoa ushirikiano kwenye zoezi la chanjo ya polio pindi litakapoanza
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa