Katika kuendeleza kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam ambayo hufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, leo Februari 25, 2023 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam CPA Amos Makalla ameiongoza kampeni hiyo kwa mafanikio ambayo kimkoa imefanyika katika wilaya ya Ubungo barabara ya Sam Nujoma.
Kampeni hiyo ni mahsusi kwaajili ya kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika kwa ujumla katika maeneo yote ili kutokuruhusu mlipuko wa magonjwa pamoja na muonekano mbaya wa viunga vya jiji la Dar es Salaam
Awali mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba amempongeza Mhe. Makalla kwa maono yake makubwa kwenye suala la usafi wa Mazingira na wao kama uongozi wa Wilaya ya Ubungo watahakikisha wanakuwa wa kwanza kwenye kuendeleza na kutafsiri kwa vitendo kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam.
Nae mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla amechukua nafasi hiyo kuipongeza Wilaya ya Ubungo kwa hamasa kubwa waliyonayo kwenye suala la usafi na mwitikio mkubwa waliouonesha leo.
"Niseme tu naupongeza uongozi wa Wilaya na Manispaa ya Ubungo kwa jinsi mnavyojipanga linapokuja suala la usafi kiukweli hamjawahi kuniangusha. Ubungo kwenye usafi siku zote imekuwa ya kwanza na huo ndio mwelekeo tunaoutaka kwa jiji letu la Dar Es Salaam" Alisema Makalla
Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa AMOS MAKALLA akipanda mti katika zoezi la usafi
Vilevile Mhe. Makalla ameendelea kuwakumbusha wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga kuwa bado ni marufuku kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ikiwema pembezoni mwa barabara, juu ya mitaro ya maji, njia za wapita kwa miguu pamoja na maeneo ya mbele kwenye taasisi za umma
Kwa upande mwingine Mhe. Makalla amemuagiza mkuu wa wilaya ya Ubungo pamoja na mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kuhakikisha wanatatua changamoto ya soko la Mawasiliano ili kuzuia wananchi kutoka nje ya soko hilo kwaajili ya shughuli zao
Aidha wadau mbalimbali wameshiriki kwenye zoezi hilo ikiwemo benki ya NMB, taasisi isiyo ya kiserikali ya HUDEFO
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa