Ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani iliyoanza tarehe Agosti 1, 2022 na itamalizika tarehe agosti 7, 2022 Manispaa ya Ubungo imetembelea kituo Cha afya Kimara ambapo Wakina mama mbalimbali waliokuja kupata huduma( clinik) wamepewa elimu kuhusu lishe ya mtoto na umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama yanayomwezesha kukua vyema kiafya
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na Kauli mbiu ya CHUKUA HATUA ENDELEZA UNYONYESHAJI; ELIMISHA NA TOA MSAADA
Akitoa elimu kwa wamama hao Bi. Jane Mbwilo Afisa lishe katika kituo Cha afya Kimara alisisitiza juu ya Faida mbalimbali zinazopatikana endapo mama atanyonyesha mtoto vizuri bila ya kumpa maziwa mengine ikiwemo kuweka ukaribu wa mama na mtoto na kuongeza upendo na Afya ya akili ya mtoto
Aliendelea kwa kusema kuwa, mama pia anapata Faida kwa kuwa ni moja ya njia ya uzazi wa mpango na inapunguza uwezekano wa kupata Kansa ya kizazi
"Tunasisitiza Maziwa ya mama ni Kinga ya magonjwa mbalimbali kwa mtoto ni vyema akanyonya muda wote" alisisitiza Jane
Nae, Afisa lishe Manispaa ya Ubungo Beatrice Mossile amesisitiza unyonyeshaji wa mtoto kwani itapunguza vifo vya watoto kwa asilimia kubwa
"kiafya ni muhimu hata Kama mama amepata mimba nyingine akiwa ananyonyesha anatakiwa kuendelea kunyonyesha mpaka mimba ya mtoto mwingine itakapofikia miezi Saba" alisema hayo Mossile
Haina madhara na pia sababu ya kuacha mimba ikiwa na miezi Saba ni kwaajili ya kumwandalia mtoto ajae apate maziwa ya awali yanayotoka kwa mama yenye virutubisho"
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa