Mapema Leo tarehe 13/09/2022 Manispaa ya Ubungo imekutana na wafanyabiashara waliopanga kwenye fremu na vizimba vya Kituo cha Magufuli Bus Terminal lengo ikiwa ni kuweka mikakati juu ya ulipaji wa kodi mpya za upangishaji tofauti na zile za awali.
Kikao hicho kimejumuisha wapangaji wa Jengo la Utawala, Jengo la Abiria na Wamiliki wa Mabasi wenye ofisi za kukatisha tiketi wa Kituo hicho ambapo hapo awali gharama za upangishaji walikuwa wakilipia Tsh 40,000/= kwa square mita moja.
Akiongea katika kikao hicho
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic ameeleza kuwa ombi la wapangaji hao la kushushiwa gharama za kodi limefanyiwa kazi kwa kupunguzwa kwa kiasi ambacho ni rahisi kwa kila mfanyabiashara kulipia.
Beatrice ameendelea kueleza kuwa kodi hizo mpya zimeanza kuchajiwa kuanzia tarehe 01/07/2022 na kwamba kutokana na ushushwaji wa kodi hizo, kwa sasa kila mfanya biashara atawajibika kulipia gharama za umeme kutokana na matumizi yake kwa utaratibu utakaopangwa isipokuwa gharama za maji zitaendelea kugharamiwa na Manispaa kama ilivyokuwa hapo awali.
Akiendelea kufafanua Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Manispaa hiyo George Mzeru ameeleza kuwa kodi hizo kwa sasa zitalipwa kwa mchanganuo ufuatao Wafanyabiashara wa Jengo la Utawala kwa Sakafu ya chini (ground floor) Tsh 25,000, Floor ya kwanza Tsh 24,500, Floor ya pili Tsh 24,000 na Floor ya mwisho ambayo ni ya Tatu italipiwa Tsh 22,000.
George ameendelea kueleza kuwa kwa Wafanyabiashara wa Jengo la abiria ambalo chini Lina basement kwahivo floor ya kwanza (mezzanine floor) itakuwa Tsh 22,500, floor ya kwanza Tsh 22,000 na floor ya pili ambayo ni ya mwisho italipiwa Tsh 22,000.
Nae Mwanasheria wa Manispaa hiyo Kissah Mbila amewataka Wafanyabiashara hao kuhakikisha hadi kufikia tarehe 25/09/2022 wote wawe wameshalipia kodi ya mwezi Julai, Agosti na September 2022 na kupatiwa mkataba wake na ambae atafanya kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kissah ameendelea kueleza kuwa mfanyabiashara mwenye madeni ya nyuma ya mwezi Julai atapatiwa mkataba wa makubaliano ya malipo ya madeni yao ya nyuma kwa gharama zile zile za awali mara tu atakapo maliza malipo ya mwezi Julai hadi September
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa