- Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania SHIMISEMITA - 2022 imeendelea kuchukua sura mpya katika hatua ya Robo fainali. Mashindano hayo kitaifa yanafanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
- Katika mashindano hayo timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeshacheza michezo mitatu ambapo imeibuka na ushindi katika michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja
Ubungo 2 Vs 1 Ilala
Ubungo 1 Vs 0 Arusha
Ubungo 0 Vs 1 Kahama
- Kwa hivi sasa Timu ya Manispaa ya Ubungo imemaliza hatua ya Makundi na sasa imefuzu kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo
- Akielezea hali ya timu katika mashindano hayo Afisa utamaduni wa Manispaa ya Ubungo ndugu Kassim Semfuko amesema kikosi kipo katika hali nzuri na ari ya timu ipo juu na matumaini yao ni kuipeperusha vema fahari ya Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa