Ugeni kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara OR-Tamisemi wamefika Manispaa ya Ubungo tarehe 29.9.2021 kwaajili ya kutengeneza mwongozo wa kitaifa na kupokea maoni ya wajasiriamali juu ya namna bora ya uanzishwaji wa maeneo rasmi kibiashara
Akiongea wakati wa kikao hicho Dr.Consolata Ishebali Mkurugenzi wa Biashara ndogo na zakati (SME) aliwaeleza wajasiriamali hao dhumuni la ujio wao ambao ni kutengeneza mwongozo na kusikiliza changamoto zao Kama wajasiriamali wadogo pamoja na kuyapokea mapendekezo yao
Nishukuru tumeona Hali halisi na wengi wenu mmezungumzia uhitaji wa mazingira rafiki kibiashara na niwaaidi tunaenda kuyafanyia kazi changamoto zenu zote ikiwa ni moja ya agizo la serikali kuhakikisha wajasiriamali wote wanapata sehemu salama zakufanyia biashara
Aidha kiongea kwa niaba ya Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Ubungo Rose Mpeleta ameushukuru Uongozi wa machinga na ugeni kutoka wizarani kwa kuweza kuwasikiliza changamoto za wajasiriamali hao wadogo wa Wilaya ya Ubungo ikiwa ni njia moja wapo wa kero kufikishwa katika mikono sahihi kwaajili ya utatuzi
Nae mwakilishi wa wajasiriamali hao wamewashukuru viongozi kwa kuweza kuwasikiliza kero zao na kuwaomba kuweza kupatiwa maeneo rafiki ambayo hayata warudisha nyuma kibiashara na hata kiuchumi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa