Leo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori amepokea ugeni wa wawakilishi kutoka World Bank Ndg. Waleed Malik na Clara Maghani na Jaji Mkuu wa Ethiopia Meaza Mengistu ofisini kwake Luguruni.
Wageni hao pia waliambatana na baadhi ya watumishi wa Mahakama kuu kama Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri ya Mahakama Tanzania Victoria Nongwa
Lengo kuu la wageni hao likiwa ni kujionea namna Mahakama inayotembea (Mobile Court) inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi.
Ikumbukwe kuwa World Bank ndio waliodhamini mradi huo na nchi ya Ethiopia iko katika mpango wa kuanzisha Mahakama hiyo ambayo hutembea kusikiliza kesi za wananchi na kuzitatua na hata kutoa ushauri wa kisheria na ndio maana wamekuja kujionea inavyofanya kazi ambapo kwa leo ilikuwa Wilaya ya Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa