Leo Oktoba 13, 2022 Mkuu wa Wikaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ametembelea ujenzi wa ofisi ya Udhibiti Ubora katika eneo la Kwembe Manispaa ya Ubungo
- Akiongea katika ziara hiyo, Mdhibiti Ubora wa Manispaa ya Ubungo Bi. Marrietha Mkai amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa ofisi hiyo kwa Manispaa ya Ubungo ambapo tayari wameshapokea jumla ya shilingi Milioni 181 kwaajili ya ujenzi huo
- Nae Mkuu wa Wilaya ya Ubungo akiongea katika ziara hiyo amezipongeza kamati zote zinazohusika na ujenzi wa ofisi hiyo chini ya Mdhibiti ubora wa Manispaa ya Ubungo. Pia amesisitiza kuhakikisha ofisi hiyo inajengwa mpaka kukamilika kwa kuzingatia ubora ili kuilinda dhamira ya Dhati ya Mhe. Rais ya kuhakikisha elimu yenye ubora inatolewa kwa wanafunzi wote kwa shule za msingi na shule za sekondari
- Ujenzi wa Ofisi hiyo unategemewa kwenda kuongeza ufanisi, uadilifu na tija ya utoaji elimu kwa shule za msingi na shule za sekondari ambapo ofisi ya udhibiti ubora ndo msimamizi mkuu wa kiwango cha elimu katika Manispaa ya Ubungo na maeneo mengine
- Nao wadau wengine wa Elimu ndani ya Manispaa ya Ubungo ikiwemo kutoka shule ya Greenbelt Schools wamechangia mifuko 100 ya saruji kwaajili ya ujenzi huo na pia mwakilishi kutoka benki ya NMB wameonesha nia ya dhati ya kuchangia ujenzi huo wakati wowote kutoka sasa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa