Wakati serikali inaendelea kujenga hospitali na vituo vya afya kote nchini, suala la kuongeza usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwenye vituo hivyo ni mhuhimu sana ili viweze kujiendesha vyenyewe hususani kununua dawa na vitendanishi badala ya kutegemea MSD na fedha kutoka kwa wahisani.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu waziri OR-TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo John Dugange leo januari 5, 2021 wakati wa Ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam na kueleza kuwa bila kuongeza usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya kutolea huduma za afya tatizo la ukosefu wa dawa linaweza kuwa kubwa.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe Dkt Festo John Dugange (aliyevaa koti) akitoa maelezo wakati alipotembelea ujenzi wa kingo za mto ng'ombe eneo la Ubungo Maji leo januari 5, 2021
Amesema serikali imetumia fedha nyingi kujenga miundombinu bora ya afya hivyo ni jukumu la viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanasimamia vituo kukusanya mapato ya kutosha ili vituo hivyo viweze kujiendesha vyenyewe hasa kwenye ununuzi wa dawa na vitendanishi.
Dkt. Dugange ameendelea kueleza kuwa"Lazima tuongeze usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na matumizi kwenye hosipitali, vituo vya afya na zahanati kwa kuziba mianya yote inayovujisha mapato kwa kutumia mbinu za kisasa za matumizi ya mifumo ya kielektroni ili mwananchi asikose dawa kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya"
Aidha Dkt Dugange ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kutekeleza kwa viwango mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya na kuagiza hospitali hiyo kukamilika na kuanza kutumika ifikapo machi mwaka huu kwani muda wa kukamilisha ulipaswa kuwa mwezi januari 2021.
"Nawapa miezi miwili tu ujenzi uwe umekamilika na huduma zianze kutolewa, wananchi wa hamu ya kuitumia hospitali yao ukizingatia vituo vya afya vilivyopo manispaa ya Ubungo vimamsongamano mkubwa sana wa wateja" aliagiza Dkt. Dugange
Dkt Dugange ameendelea kuipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kufanikiwa kukusanya bilioni 9.1 kati ya bilioni 18 iliyokasimiwa kukusanya kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambayo ni asilimia 51 ya mapato yake ya ndani hadi kufikia desemba 2020 na kufanikiwa kutumia zaidi ya bilioni 3 kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madaraza, vituo vya kutolea huduma za afya na kupeleka 10% kwenye mfuko wa wanawake, vijana na walemavu.
Kuhusu juhudi za kupunguza tatizo la mafuriko na foleni jijini Dar Es salaam, serikali imetumia zaidi ya bilioni 55 kujenga kingo kwenye mto sinza na mto ng'ombe ili kupunguza athari za mafuriko kwa wananchi pamoja na kujenga barabara ya kilomita 18 kwa ajili ya kupunguza kero ya foleni.
Barabara ya Shekilango ikiwa kwenye hatua za mwisho za umaliziaji na wananchi wakiendelea kunufaika nayo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa