Diwani wa Msigani Mhe.Siraju Mwasha ameweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Temboni iliyopo mtaa wa Temboni kata ya Msigani ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na fedha kutoka Manispaa ya Ubungo Shilingi milioni 15 na Serikali kuu shilingi milioni 62
Zahanati hii ni muhimu sana kwa wananchi wa maeneo haya kwani kwa sasa huduma za Afya wanazipata kupitia zahanati ya Malamba mawili pamoja na kituo cha Afya cha Mbezi
Diwani kata ya msigani Siraju Mwasha akiweka jiwe la msingi katika zahanati ya temboni
Malengo ni kuhakikisha Zahanati hii inaanza kutoa huduma zake kwa Wananchi mwezi Machi 2023 ili kugatua huduma ya afya kwa ukubwa zaidi kwa wananchi wa maeneo haya
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa