Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe.Kitila Mkumbo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo tarehe 18/9/2021 amepokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo Cha Biashara na Vifaa vya Afrika Mashariki ambao kampuni ya shangai linghang Group itaufanya katika eneo la Ubungo ambapo stendi ya zamani ya mabasi ilikuwepo
Akisoma taarifa ya mradi mbele ya viongozi wa mbalimbali wa serikali Director wa Kampuni shangai Linghang Cath Wang alisema kuwa kampuni hiyo ya kichina inategemea kufungua Kituo Cha Biashara na Vifaa vya Afrika Mashariki ambacho kitatoa huduma kwa watanzania wote na kutengeneza fursa mbalimbali kwa watanzania
Aliendelea kwa kusema kuwa ujenzi wa mradi huo utakamilika kwa muda wa miezi 15 na Utakuwa na gharama zaidi ya billioni 260 za kitanzania na utakapomalizika unaweza kutengeneza fursa ya ajira kwa takribani watu elfu 20 pia kusaidia halmashauri kuweza kukusanya mapato na kuwa kivutio katika Wilaya ya Ubungo kwa ukubwa na ubora wake
Aidha kitila amesema kuwa ni mradi ambao utakuwa na tija na manufaa kwa watu wa Ubungo na watanzania kwa ujumla kwa kuweza kurahisisha upatikanaji wa huduma hata kuleta manufaa kwa serikali na hasa katika ukusanyaji wa mapato ambao halmashauri itaenda kunufaika
Aliendelea kwa kuwapongeza na kuwaasa kampuni hiyo kuzingatia vigezo ambavyo viongozi mbalimbali waliweza kuvisema ili kuleta maboresho katika taarifa yao waliyoisoma ikiwemo uzingatiaji wa vigezo vilivyotolewa
Aidha mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ameishuru kwa kampuni hiyo ambayo inaenda kutengeneza fursa kwa Wana Ubungo na pia Manispaa kuongeza mapato yake kupitia mradi huo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa