Ubungo imezinduzi rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya polio katika Hospitali ya Sinza Palestina ikiwa ni awamu ya tatu ya utoaji wa chanjo hiyo na zoezi Hilo litaendelea kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Leo tarehe 1 Hadi 4 septemba, 2022
Kwa Wilaya ya Ubungo watoto 174,588 wanalengwa kufikiwa na Katika kuhakikisha huduma inawafikia wananchi kwa haraka. Wataalamu wa Afya watapita nyumba kwa nyumba na pia katika Vituo vyote vya Afya chanjo tayari imesambazwa.
Akizindua zoezi hilo Leo tarehe 1 septemba, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amewasihi Wakina mama kuhakikisha watoto wanapata chanjo hiyo kuwaepusha watoto na ugonjwa wa kupooza
"Wananchi wetu tutawafikia popote walipo, wahudumu wetu wa Afya watapita kuhakikisha zoezi hili linafanyika" alisema hayo Kheri
Kheri Aliendelea kuwasisitiza wakina mama hao kuhakikisha wanazingatia usafi wa maeneo yao kwa kunawa mikono na maji safi na kuweka makazi yao safi ili kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa