Katika kuhakiksha masoko yanaleta tija kwa serikali na wafanyabiashara kama chanzo cha mapato, soko la SIMU2000 lililopo kata ya sinza Manispaa ya Ubungo limeanzisha programu ya gulio kila Siku ya ijumaa ya wiki lengo ikiwa ni kulitangaza soko hilo na hatimaye kupata wafanyabiashara wapya katika soko hilo.
Uzinduzi huo kufanyika leo januari 8,2020 ambapo wafanyabiashara na wanujuzi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es salaam wamepata fursa ya kuuza na kununua bidhaa Mbalimbali katika gulio hilo.
Akizungumza na wanunuzi na wafanyabiashara wasiofika katika soko hilo, Afisa Biashara wa Manispaa ya Ubungo Prisca Mjema amewapongeza kwa mwitikio mkubwa walioonesha ikiwa ni Siku ya kwanza ya kuanza gulio hilo.
"Nawapongeza sana kwa mwitikio huu , imeonesha uthubutu wenu katika kufanya biashara na imenitia nguvu sana mimi kama msimamizi wa masoko na biashara zingine kuona huu ulikuwa ni uhitaji mhimu kwa wafanyabiashara, hivyo tunaahidi kuendeleza Gulio hili" alisema Mjema
Mjema amefafanua kuwa soko la SIMU2000 ni soko ambalo lipo sehemu nzuri linafikika kiurahisi hivyo wafanyabiashara tukiungana pamoja tunaweza kulifanya soko hili kuwa na gulio kubwa la mfano kwa jiji la Dar Es salaam
Muonekano wa Gulio katika Soko la SIMU2000 lililozinduliwa leo
"Tuendelee kuwatangazia wafanyabiashara wengine wa maeneo tofauti waje kufanya biashara katika soko letu, hii atafanya wateja wengi kuja kununua bidhaa Mbalimbali katika soko hili hatua hiyo itapelekea kutafsiri kwa vitendo dhana ya uwepo wa masoko na ukuzaji uchumi "
Kwa upande wake Unick Mrango ambaye ni mfanyabiashara katika soko hilo kwa zaidi ya miaka mitano ameshukuru Manispaa ya ubungo na uongozi wa soko kubuni mbinu ya kuwa na Gulio kwenye soko hilo kwani limefanya soko lichangamke na wafanyabiashara wameuza sana tofauti na siku za kawaida.
Kutokana na mwamko huo Unick ameshauri gulio hilo lifanyike kwa Siku mbali badala ya siku moja kwa wiki kwa sababu linakutanisha wafanyabiashara wenye bidhaa tofauti hali inayovutia wateja wengi kuja kununua lakini pia tutatangaza soko vizuri zaidi.
Aidha kupitia gulio hilo biashara ambazo zilikuwa hazionekani zimeweza kuonekana hata wateja wamegundua kuwa ndani ya soko kuna bidhaa kwani mwanzo wengi walikuwa hawajui kuwa ndani kuna soko kubwa anasema Unick.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa