Kamati ya Sensa ya Majaribio Wilaya ya Ubungo yazinduliwa rasmi tarehe 17.9.2021 ambayo tayari imeshapatiwa mafunzo kwaajili ya kuendelea na zoezi la kuhesabu watu na makazi ambayo hufanyika kabla ya sensa kamili itakayofanyika mwaka 2022
Lengo la kamati hizo ni kusimamia kazi za sensa kwa ujumla katika maeneo yao, kutoa ushauri wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya sensa, kuitangaza sensa kwa maana ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa sensa pamoja na umuhimu wa Kila mtu kuhesabiwa,
Na pia kutekeleza majukumu ya kupokea na kusimamia utekelezaji wa miongozo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kutoka katika kamati ya sensa mkoa na kushiriki katika kuhamasisha watu wakati wa maandalizi ikiwa ni pamoja na wakati wa kutenga maeneo ya kijiografia na wakati wa kuhesabu watu. n.k
Akizindua rasmi kamati hiyo Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanafanya zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa ili Wilaya ya Ubungo iwe mfano katika utekelezaji wa zoezi hilo
Mkazingatie majukumu yenu ili serikali iweze kupata takwimu kamili ambayo itaweza kutumika katika kuleta maendeleo
kwa Wilaya ya Ubungo zoezi hili litafanyika katika kata ya manzese mtaa wa chakula Bora na kuhimiza kuhakikisha waratibu wanawapa elimu wananchi ambayo itawafanya waweze kutoa ushirikiano mzuri ili kufikia lengo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa