Uzinduzi wa kampeni ya Usafi kiwilaya umefanyika katika kata ya Msigani eneo la Stendi ya daladala ya Malambamawili leo disemba 04, 2021
Kampeni hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James akiambatana na Viongozi Mbalimbali pamoja na wananchi kufanya usafi katika eneo hilo na kuwaeleza wananchi kuwa suala la usafi liwe la kila siku kuanzia mtu binafsi hadi taasisi.
"Lengo la kampeni hii ni kuweka mji wetu Safi na kujikinga na magonjwa yanayotokana na uchafu, hivyo kila mmoja aone ana wajibu wa kufanya usafi na kitotupa taka ovyo na kampeni hii ni endelevu" ameleleza Mhe. Kheri
Kampeni hii inaongozwa na kaulimbiu isemayo SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM inayolenga kuweka jiji Safi na kulinda afya za Wananchi wake.
USAFI NI AFYA,
USAFI NI USTAARABU UNAANZA NA WEWE
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa