Vijana 50 Kati ya 100 wa Manispaa ya Ubungo waliochaguliwa kwenye mradi huo walipata mafunzo ya kujifunza Kilimo biashara cha mbogamboga, wamefuzu mafunzo hayo na kuahidi kutumia Elimu hiyo katika kujiongezea kipato kupitia Kilimo hicho cha kisasa kinachotumia eneo dogo kwa uzalishaji mkubwa.
Katika mafunzo hayo Vijana hao wamepata Elimu ya kutumia kitalu nyumba kama njia bora zaidi katika kuzalisha mazao mengi na yenye ubora na ushindani kwenye soko.
Wakizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyoendeshwa na ofisi ya Waziri Mkuu Kupitia kampuni ya SUGECO wameishukuru Serikali Kwa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kujiajiri kupitia Kilimo badala ya kukaa vijiwemi.
"Vijana wengi wanadhani Kilimo kinafanyika vijijini tu, kazi yetu mojawapo ni kubadilisha mtizamo huo potofu ili wajue kuwa hata mjini Kilimo kinalipa zaidi kwani unalima eneo dogo mazao mengi na yenye ubora". Alisema mmoja wa Vijana hao baada ya kupata mafunzo hayo.
Kwa upande wake Afisa Kilimo na umwagiliaji na ushirika Happiness Mbelle amewasisitiza vijana hao kuzingatia mafunzo waliyopewa kwani Serikali inatamani kuona Vijana wakijiajiri kupitia Kilimo.
Aidha, Mbelle amesema ili kuwawezesha Vijana hao kuonesha mafunzo hayo Kwa vitendo Halmashauri itatoa ekali tano Kwa ajili ya kuanza Kilimo Kwa vitendo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa