Jumla ya Vikundi 22 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu waliopata mikopo ya vyombo vya moto yaani Pikipiki, Toyo na Bajaji wamepewa maelekezo na utaratibu wa namna ya kununua vyombo hivyo kwa kuzingatia viwango vya ubora.
Vikundi hivyo vimepokea maelekezo hayo kutoka ldara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana ya Manispaa ya Ubungo mara baada ya kupata mkopo huo uliotolewa na Manispaa mapema Januari,2021 na kueleza kuwa vikundi vitaunda Kamati za kufanya manunuzi kadiri ya mahitaji yao sambamba na kuweka uwazi wa ununuzi huo.
Akiongea wakati wa kutoa maelekezo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana wa Manispaa ya Ubungo Bi. Rose Mpeleta ameeleza kuwa Manispaa ya Ubungo imeamua kutumia utaratibu huo ili kuvipa uhuru vikundi katika kununua vyombo hivyo na Manispaa itawajibika kuwasaidia kulipa fedha hizo kwa wazabuni husika.
"Kila chombo kitasajiliwa kwa jina la kikundi lakini Kadi zitatunzwa na Manispaa mpaka watakapomaliza marejesho kwa mujibu wa utaratibu ndipo Kadi hizo watarudishiwa" alieleza Bi. Rose Mpeleta.
Mpeleta ameendelea kuwasisitiza wanavikundi hao kuwa, baada ya kununuliwa vyombo hivyo vitakaguliwa ili kujiridhisha na viwango vya ubora kulingana na mahitaji ya wanavikundi.
Mpeleta amefafanua kuwa "Huu ni utaratibu mpya umewekwa, hapo zamani vikundi vilikuwa vinakabidhiwa fedha na kufanya manunuzi vyenyewe hali ambayo vikundi vingine vilipata vyombo ambavyo havina ubora"
Stuwart Banda ni mwanakikundi wa Kikundi cha Vijana cha Jiwezeshe kutoka Kata ya Goba ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwawezesha vijana kupitia mikopo isiyo na riba kwani inatusaidia sana katika kujikwamua kiuchumi na kutimiza malengo yao.
Aidha, Stuwart amewasii vijana kuwa wavumilivu kwenye biashara maana wengi hawavumilii changamoto, mfano kikundi chetu kilianza na wanachama 27 lakini mpaka sasa kimebaki na wanachama 8 tu na baada ya kupata mkopo huu kila mwanakikundi atakuwa anamiliki bodaboda yake.
Moja ya kikundi cha vijana (waliokaa mstari wa mbele) waliopewa mkopo wa vyombo vya moto na Manispaa ya Ubungo
Watu wenye ulemavu nao wamesitizwa kutokata tamaa kwani mikopo inayotolewa na Manispaa inawahusu pia wao, jiungeni kwenye vikundi ili mpate mikopo ya kukuza biashara zenu badala ya kukaa na kunung'unika " alieleza Mary Chibago Mwanachama wa Kikundi cha *Five Star's Disabled Group.*
Hadi kufikia Januari, 2021, Manispaa ya Ubungo imetoa mikopo isiyo na riba yenye jumla ya Shilingi bilioni 1.1 kwa vikundi 111. Mikooo hiyo ina lengo la kuviwezesha vikundi hivyo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa