Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka kata 14 za Manispaa ya Ubungo wamepata mafunzo ya namna ya kusajili vikundi vya kijamii vya huduma dogo za fedha maarufu kama VIKOBA kwa njia ya kielektroniki ili wakaelimishe vikundi vilivyopo kwenye maeneo yao na kuvisaidia katika usajili Mpya kama sheria inavyotaka
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa maafisa hayo, Afisa Maendeleo wa Manispaa ya Ubungo, Evelyne Mangwea alisema kuwa, usajili huu Mpya wa vikundi vya kijamii ni utekelezaji wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.
Usajili wa vikundi hivyo kupitia mfumo huo itarahisisha usajili, usimamizi na utoaji wa taarifa za vikundi Kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa sekta ndogo ya fedha ili kukidhi mahitaji halisi ya wananchi wa kipato cha chini na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi
Evelyne ameeleza usajili wa vikundi kupitia mfumo huo mpya wa kielektroniki utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi, udhulumaji, migogoro pamoja na kudhibiti upotevu wa fedha kwenye vikundi.
"Kuanzia tarehe mosi mei mwaka huu vikundi vyote vinatakiwa viwe vimejisajili kwenye mfumo wa kielektroniki ili ili viweze kutoa huduma za kifedha na usajili huu ni bure hivyo kila Afisa Maendeleo akahakikishe anatoa elimu ya usajili huu kwa vikundi vilivyopo kwenye kata yako" alieleza Evelyne.
Evelyne ameendelea kufafanua kuwa, Vikundi vitakavyohusika na usajili kupitia mfumo huo Mpya unaosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni vile ambavyo havijasajiliwa kisheria ili vitambuliwe na mifumo ya kifedha ya Serikali na kuhakikisha usalama wa fedha zao.
Kwa mujibu wa muingozo huu kikundi kitaweza kusajili wanachama kuanzia kumi (10) hadi hamsini (50) na sio zaidi au chini ya hapo. Aidha vikundi hivyo vitajulikana kwa jina la Community microfinance Groups ( CMGs) badala ya jina la VICOBA lililozoeleka.
Akielezea namna ya kutumia mfumo huo wa usajili, Afisa Tehama wa Manispaa hiyo Aziza ameeleza kuwa baada ya kupatiwa elimu ya namna ya usajili, wanachama watajisajili wenyewe kwa kutumia komputa au simu za rununu na Afisa Maendeleo ngazi ya kata atapata fursa kuvisaidia vikundi katika zoezi la usajili ikiwemo kuhakikisha nyaraka zinazotakiwa zinapakiwa kwenye mfumo pamoja na kuona vikundi vinavyojisajili.
Akiongea kwa niaba ya maarifa maendeleo waliohudhuria mafunzo hayo, Ramla Mustafa Afisa Maendeleo wa kata ya Ubungo amesema watajitahidi kuwaelekeza wanavikundi kujisajili kupitia mfumo you mpya ili waweze kuendelea na shughuli zao za kuwezeshana kiuchumi pamoja na kufuatia sheria za nchi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa