Manispaa ya Ubungo imetoa mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamali 133 vya wanawake, vijana na watu ulemavu watakaopata mkopo usio na riba wa Tsh bilioni 1.1 kupitia asilimia 10 ya mapato yake ya ndani lengo ikiwa ni kuwezesha vikundi hivyo kuweza kujiajiri kupitia shughuli zao za kiuchumi.
Akizungumza katika mafunzo hayo yatakayo fanyika katika siku mbili Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo Rose Mpeleta alieleza kuwa Halmashauri imeiona itoe mafunzo elekezi kwa vikundi hivyo ili kuvisaidia kufanya matumizi ya pesa hizo sawa na malengo ya fedha hizo na si vinginevyo na sio kufanyia shughuli nyengine
“Nawasisitiza baada ya kupata mikopo hii tumieni kuwekeza kwenye biashara za kiuchumi na kukumbuka kutoa marejesho ili kuwapa wengine fursa ya kupata mikopo hiyo na sio kwenda kufanyia shughuli za sherehe za kujiturahisha”.
Mpeleta amefafanua kuwa jumla ya vikundi 133 vyenye wajasiriamali wapatao 1,201 wanaenda kupatiwa mikopo yenye jumla ya Tsh Bilioni 1.1 ikiwa vikundi vya wanawake 85 watapatiwa jumla ya Tsh Milioni 643 vikundi vya vijana 42 watapatiwa Tsh Milioni 429.4 na Tsh Milioni 74 zitatolewa kwa vikundi 6 vya watu wenye ulemavu.
Aidha katika mafunzo hayo wawezeshaji wametoa mafunzo ya uongozi bora wa miradi, usimamizi wa fedha, uendeshaji wa miradi na itoaji taarifa kuhusiana na mikopo hiyo ikiwa ni kusaidia vikundi hivyo kwenda kuendesha vyema miradi yao na kusaidia kurejesha fedha kwa wakati.
Nae Mh Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga ameishukuru Manispaa kwa fedha hizo kwani zitaenda kuwapa heshima katika uongozi wao na amempongeza Afisa Maendeleo wa Manispaa hiyo kwa jitihada anazozifanya katika kuhakikisha vikundi hivyo vinapata mikopo.
Akiongea kwa niaba ya wanufaika wa mkopo huo ndugu Ereneo Pelagi Mushi ameishukuru Manispaa na Serikali kwa ujumla kwa mikopo hiyo na kuwashauri vijana, wanawake na walemavu wengine pia waweze kujiunga na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali ili kuweza kupata fursa ya mikopo hiyo isiyo na riba ambayo itaenda kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa