Wakala wa barabara za vijijini na mijini Tanzania (TARURA) imetoa mafunzo elekezi kwa viongozi wa Wilaya ya Ubungo wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama, Madiwani na Wataalamu juu ya uanzishwaji wa mfumo mpya wa kielektroniki wa kukusanya ushuru wa maegesho unaoitwa TeRMIS App ikiwa ni mkakatibwa kuongeza mapato na kuboresha miundombinu ya barabara
Akitoa ufafanuzi malengo ya kuanzisha mfumo huo Geofrey Mkinga meneja wa TARURA Mkoa wa Dar Es Salaam alisema kuwa utaongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya serikali yatakayosaidia kuboresha maendeleo ya barabara na kusaidia wateja kufanya maombi na kulipia huduma bila kufika ofisi za TARURA hali itakayopunguza usumbufu kwa wateja.
Mkinga amesema kuwa mfumo huo utaanza kutumika rasmi Desemba 1, 2021 hivyo watumiaji wote wa vyombo vya moto wajiandae kuanza kutumia mfumo huu ambao ni rafiki na rahisi zaidi.
Kuhusu gharama za ushuru wa maegesho hayo ,Mkinga ameeleza kuwa mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa tsh 500/= kwa saa na tsh 2,500/= kwa siku
Mkinga ameendelea kueleza kuwa , mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa ushuru wa maegesho ndani ya siku 14 tangu alipotumia Maegesho na endapo atashindwa kulipa ndani ya muda huo anatakiwa kulipa ushuru wa maegesho pamoja na faini ya tsh 10,000/=. Aidha wananchi wanapaswa kujua mwisho wa mipaka ya maeneo yao na kuacha kutumia maeneo ya TARURA kiholela pia wanapaswa kujua kuwa fedha za ushuru wa maegesho zinazokusanywa na wakusanya ushuru ni za serikali na sio zao binafsi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ndugu Kheri James amewapongeza TARURA Kwa kuweza kuanzisha mfumo huo wenye kuleta tija kwa jamii.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa