Viongozi wa mitaa 50 Manispaa ya Ubungo inayotekeleza mradi wa kunusuru kaya kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wameagizwa kuhakiki walengwa wanaonufaika na mfuko huo ili kuhakikisha kaya zisizostahili maarufu kama Kaya hewa zinaondolewa kwenye mpango huo.
Agizo hilo limetolewa leo januari 8, 2021 na Mratibu wa TASAF Manispaa ya Ubungo Wakuru Nyaratha wakati alipofanya ziara ya kutembelea viongozi hao na kueleza kuwa zoezi hilo la uhakiki ni mwendelezo wa uhakiki uliofanyika mwezi julai na novemba mwaka 2020 lengo ikiwa ni kuhakikisha mpango huo unanufaisha walengwa halisi.
Wakuru amefafanua kuwa uhakiki uliofanyika awali mwezi julai na mwezi novemba mwaka 2020 kaya zote zilizobainika kukosa sifa ziliondolewa kwenye mfumo wa ruzuku ya TASAF hivyo uhakiki wa sasa ni kujiridhisha zaidi endapo kuna kaya isiyo na sifa na bado inanufaika na mpango.
Wakuru amesema kuwa "muongozo wa TASAF unataka kaya zinazonufaika zisiwe kaya za viongozi wa serikali za mitaa, wastaafu, waajiriwa na watu wenye vipato vya kujitoshereza"
Baada ya uhakika wa mwezi julai na novemba 2020, Manispaa ya Ubungo ina jumla ya kaya 2189 zinazonufaika na mfumo wa ruzuku kwa walengwa TASAF wa kati ya kaya 2656 zilizokuwepo awali. Aidha katika uhakiki kaya 20 zilihama makazi, kaya 16 zilijitokea kwa hiari huku kaya 11 zikipoteza sifa kutokana na kifo, kaya 400 hazikujitokeza kwenye uhakiki.
Kwa upnde wake, Diwani wa kata ya Goba Mhe. Ester Radislaus Ndoha amekiri kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya kaya zisizo na sifa kunufaika na rukuzu inayotolewa na TASAF huku wale wanaostahili kukosa fursa hiyo.
"Nitasimamia kuhakikisha tunafanya uhakiki makini ili kaya zisizo na sifa wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa ziondolewe kwenye mpango kama muongozo unavyotaka, lakini pia kumuunga mkono mheshimiwa Rais ambaye anataka mpango huu uwasaidie wale wasiojiweza kiuchumi angalau wawe na uhakika wa kupata mahitaji ya msingi.
Kwa malipo ya mwezi wa Oktoba, kaya jumla ya shilingi 137,034,000 zilitolewa kwa kaya 1595.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa