Dunia inahama kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia na katika eneo la elimu ni muhimu sana kuendana na teknolojia ili kupata uwiano mzuri wa kuboresha huduma ya elimu. Hayo yamesemwa leo Januari 16, 2023 katika ukumbi wa Anazak na mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James wakati anakabidhi vishkwambi 3354 ambapo Vishkwambi 2162 ni kwa shule za msingi na Vishkwambi 1192 ni kwa shule za sekondari ili kuongeza tija ya utoaji elimu bora.
Mhe. James amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuelekeza vishkwambi hivyo wapewa walimu, hivyo basi ni matarajio yake kuona vishkwambi hivo vinaongeza tija kubwa kwenye kuongeza ufaulu"Mhe. Rais ana matarajio makubwa sana kwenu. Nendeni mkawasimamie vizuri walimu wenu kwenye matumizi sahihi ya vushkwambi hivo. Kwa kufanya hivo tutakuwa tumemuunga mkono Rais kwa vitendo" Alisema James
MKUU WA WILAYA KHERI JAMES AKIMKABIDHI KISHIKWAMBI MMOJA WA WALIMU KATIKA ZOEZI LA UGAWAJI WA VISHIKWAMBI KWA WALIMU
Akiongea katika hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Elimu sekondari Manispaa ya Ubungo Ndugu Voster Mgina amesema kuwa walimu wote wa Manispaa ya Ubungo watakabidhiwa vishkwambi hivo kila mmoja kwa maelekezo ya kuvitumia kwenye shughuli zao za kikazi ikiwemo kuhifadhi taarifa, kutafuta maarifa pamoja na kufundishia
Kwa upande wa walimu hao wakuu wamemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa vishkwambi hivo na wameahidi kuvitunza na kuvisimamia vizuri ili vilete matokeo
WALIMU KATIKA PICHA YA PAMOJA KATIKA ZOEZI LA UPOKEAJI WA VISHIKWAMBI
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa