Viongozi mbalimbali wa vyama rafiki vya kisiasa Wilaya ya Ubungo wamefika katika shule ya Msingi Kingo'ngo kuchangia nguvu kazi katika ujenzi wa madarasa 9 unaendelea shuleni hapo.
Viongozi hao wametoka Chama cha democrasia makini, NRA, UDP , CCK, UMD na Ada-tadea Wakizungumza kabla ya kuanza kazi hiyo wamesema, lengo lao ni kuongeza nguvu katika ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule hiyo
Aidha wamesema "Maendeleo hayana Chama, Uchaguzi umeisha Kwa sasa tufanye kazi Kwa maendeleo ya wananchi" Viongozi hao wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano Katika mradi huo mpaka Utakapokamilima
Pia wamesema kuwa wapo tayari kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo
Ujenzi wa madarasa 9 shule ya msingi king'ongo iliyopo kata ya saranga Manispaa ya Ubungo .
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa